Malala Yousaf Zay alifika nchini Uingereza jana baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Birmingham kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Queen Elizabeth mjini humo.
Mganga mkuu wa Hospitali hiyo, David Rossi ameeleza matumaini yao juu ya Hali ya Malala.
Malala alipigwa risasi na Taliban wakati akirejea nyumbani toka shuleni kwenye bonde la Swat ambalo awali lilikuwa likidhibitiwa na kundi la wanamgambo wa Taliban, ikiwa ni adhabu kwa kile kilichoelezwa kushiriki kwake binti huyo katika kampeni za kuhamasisha maswala ya haki ya elimu kwa mtoto wa kike.
